Baada ya milango ya uhamisho kufungwa, ligi mbalimbali barani Ulaya zilijinyakulia wachezaji wenye tajiriba ya juu kwa kiwango cha hela walizozitenga. Timu za Ligi kuu ya Uingereza ndizo ziliotumia hela nyingi kwa ununuzi wa wachezaji kati ya Ligi kutoka Uispania, Ujerumani, Ufaransa na Itali.
Katika ligi ya Uingereza klabu ya Manchester United ndio iliyovunja rekodi ya ununuzi kwa kuwasajili wachezaji ghali zaidi akiwemo Paul Pobga kwa kima cha Euro milioni 105 na Henrikh Mkhitarya kwa Euro milioni 42. Manchester City nao walijikwamua na kuwachukua John Stones na Leroy Sane kwa Euro milioni 55.6 na Euro milioni 50 mtawalia. Arsenal almaarufu “The Gunners” waliweza kumnunua Granit Xhaka kwa Euro milioni 45 katika msimu wa uhamisho.
Ligi kuu ya Italia imeorodhesha majina makuu ya wachezaji wakihamia katika vilabu vya kandanda nchini humo. Majina makubwa kama Gonzalo Higuain ni mmojawapo wa wachezaje ambao aliyesajiliwa na Juventus kwa kitita cha Euro milioni 90. Wengine walio sajiliwa Juventus kwa hela za kutamanika ni Miralem Pjanic na Marko Pjaca kwa Euro million 32 na 23 mtawalia. Timu ya Inter Milan ni ya pili katika vilabu vya Italia iliyogharamika kusajili huduma za Joao Mario na Gabriel kwa Euro milioni 40 na 27.5.
Bundesliga imeorodheshwa ligi ya tatu kutumia hela nyingi katika uhamisho uliokamilika. Bayern Munich walitumia Euro milioni 70 kuwanunua Mats Hammels na Renato Sanches. Timu nyengine zilizokaribia miamba hao wa Ujerumani Bayern Munich ni Dortmund na Schalke 04. Dortmund waligharamika Euro milioni 52 ili kupata huduma za Andre Schurrle na Mario Gotze. Schalke 04 walitumia Euro 27.5 kwa huduma za Breel Embolo.
Miamba wa Uspania Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid ni vilabu vilivyo sajili wachezaji ghali katika ligi ya La Liga. Barcelona iliweza kuwanunua Andre Gomez, Paco Alcacer na Samuel Umtiti kwa jumla ya kitita cha Euro milioni 90. Real Madrid na Atletico Madrid wote waliweza kutumia Euro milioni 30 na 32 kila timu kwa Alvaro Morata na Kevin Gameiro.
French Ligue 1 imefunga udhia ya ligi tano zilizotumia hela nyingi katika uhamisho wa wachezaji. PSG na Monaco ndizo timu zilizobobea katika uhamisho katika ligi kuu ya Ufarasa, French Ligue 1. PSG waligharamika kuwasajili Grzegorz Krychowiak na Jese kwa Euro milioni 33.6 na 25. Monaco walisaka huduma za Djibril Sidibe, Benjamin Mendy na Kamil Glik kwa gharama ya Euro milioni 39.
Baada ya shughuli nzima ya uhamisho kukamilia macho yote yanaelekezwa kwa timu na wachezaji waliosajiliwa kwa hela nyingi. Kutokana na historia, msimu huu wa uhamisho ndio uliokuwa ghali ukilinganisha na misimu iliopita. Je! Vilabu vilivyosajili wachezaji ghali zaidi vitafanya vyema katika msimu huu mpya kwenye ligi mbalimbali?
Discover more from ULIZA LINKS NEWS
Subscribe to get the latest posts sent to your email.