in

Lyrics : Utamu Wa Yesu By Rose Muhando

rose eldoret 11

Below Are The Lyrics Of Utamu Wa Yesu By Rose Muhando

 

Lile lile…Acheni muone utamu wa Yesu we

Acheni muone utamu wa Yesu we 
Mama we onjeni utamu wa Yesu we 
Mwenzenu nimeonja utamu wa Yesu we 
Usione nina raha nimeonja utamu wa Yesu we

Si kama nimechanganyikiwa bali ni utamu wa Yesu we

Jamani sijarukwa na akili bali utamu wa Yesu we

Utamu we, nimeonja utamu we x2 

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2 
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3 
Utamu wa Yesu we, he 
Mwemere, mwemere x4 (?)

Viko vingi vitamu lakini mwisho wake mauti 
Viko vingi vitamu lakini mwisho wake kilio
Vingine ni vitamu lakini mwisho wake kilio
Ni vitamu lakini mwisho vichungu kama shubiri
Ni vitamu lakini mwisho vinawasha kama upupu
Ni vitamu lakini mwisho vinapalia we 

Acheni niuseme utamu wa Yesu we 
Wacheni nisifu utamu wa Yesu we
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we
Haufanani na utamu wa asali, utamu wa Yesu we
Thamani yake imeshinda almasi, utamu wa Yesu we
Ni mali ghafi isiopatika kwa mapesa jamani he
Bali kwa njia ya msalaba tumepewa utamu wa Yesu we
Mbinguni tunakwenda bure, uzima tunapata bure
Wokovu tumepata bure, amani tunapata bure
Utamu we, nimeonja utamu we x2 

(Chorus)

Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we

Usione tuna raha, tumeonja utamu wa Yesu we

Usione tunacheka, tumeonja utamu wa Yesu we

Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we

Umetusogeza karibu na Mungu, utamu wa Yesu we

Dhambi zetu zimewekwa mbali na Mungu, utamu wa Yesu we

Walio chini wameinuliwa, utamu wa Yesu we

Badala ya kilio ni kicheko, utamu wa Yesu we

Badala ya aibu utukufu, utamu wa Yesu we

Mito ya baraka inatiririka, utamu wa Yesu we x2

Utamu we, nimeonja utamu we

(Chorus)

Mkitaka magari mazuri, onjeni utamu wa Yesu we

Mkitaka majumba mazuri, onjeni utamu wa Yesu we

Mkitaka kubarikiwa, onjeni utamu wa Yesu we

Mkitaka kuinuliwa, onjeni utamu wa Yesu we

Utamu we, nimeonja utamu we

(Chorus)

Sing’oki ng’o, kwa Yesu sing’oki ng’o x4
Utamu we, utamu x3 
Utamu wa Yesu we


Discover more from ULIZA LINKS NEWS

Subscribe to get the latest posts to your email.

Written by Link Press

Uliza Links Team
Email :info@ulizalinks.co.ke
Phone : 0727041162
CPT HSE, Forest Road, Parklands

Kenya High Court Rules That SDA Students To Be Allowed To Go Church On Saturdays

4 Facts That The World Is In The Church